Jumapili 8 Februari 2026 - 19:00
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi atoa tahadhari kuhusiana na kulinganisha alama za kudhihiri

Hawza/ Kwa masikitiko, mojawapo ya changamoto kubwa katika suala la Mahdawiyya ni kuenea ulinganisho wa alama za kudhihiri kwa mtazamo wa kijuujuu na usio na msingi wa kielimu; mtazamo wa upotofu ambao katika historia umeandaa mazingira ya kujitokeza  wanaodai uongo na kuuweka pembeni ukweli halisi wa dhana ya kusubiri kudhihiri.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hapa tunarejea sehemu ya hotuba ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu suala la kulinganisha alama za kudhihiri, iliyotolewa mbele ya wataalamu wa masuala ya Mahdawiyya.

Kulinganisha alama za kudhihiri; ndiyo au hapana?

Mojawapo ya hatari kubwa katika mada ya Mahdawiyya ni vitendo vya kijuujuu, vya kijahili, visivyo na ushahidi na vinavyotegemea mawazo na dhana za kubuni, ambavyo vinaandaa mazingira ya kujitokeza wanaodai uongo na kuwafanya watu wawe mbali na ukweli halisi wa kusubiri kudhihiri.

Katika historia, kumekuwa na watu waliolinganishwa na baadhi ya alama za kudhihiri au waliojaribu kuzilinganisha alama hizo kwao au kwa wengine. Mambo yote hayo ni ya makosa na ya upotofu, kwa sababu sehemu ya riwaya kuhusu alama za kudhihiri haina uthibitisho wa kuaminika au ni dhaifu, na hata yale yaliyo sahihi hayawezi kulinganishwa kirahisi na matukio au watu fulani.

Mambo haya ya makosa na ya upotofu husababisha ukweli wa msingi wa Mahdawiyya na dhana ya kusubiri kudhihiri kupuuzwa. Kwa hiyo, ni lazima kuepuka kwa nguvu zote vitendo na uvumi wa kijuujuu.
(18/04/1390)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha